Saturday, November 4, 2017

Dawa ya asili ya fangasi Ukeni

DAWA YA ASILI YA FANGASI UKENI
Fangasi ukeni ni muwasho sehemu ya ndani ya uke ambao unaweza kuambatana pia na kuvimba kwa uke. Leo sitaongelea sana juu ya nini kinasababisha hizi fangasi sehemu ya uke bali tutaona dozi kamili ya asili inayoweza kutibu kabisa tatizo hili linalosumbuwa wanawake wengi miaka sasa.
Tumia dawa hizi 3 zote kwa pamoja ili kupata matokeo mazuri na usiache kuleta mrejesho hapa namna unavyoendelea:
1. LEMONADE
Lemonade inaandaliwa kwa kutumia limau, maji, asali na mdalasini ya unga kidogo, nayo inaandaliwa hivi:
*Chukua asali mbichi nusu Lita
*Chukua limau kubwa 12 au zaidi, zikate katikati kila moja. Zikamuwe moja baada ya nyingine kupata maji maji ya limau mpaka umepata ujazo wa nusu lita.
*Kwenye sufuria nyingine kubwa changanya mdalasini ya unga vijiko vikubwa 10 na maji lita 2 na nusu na uchemshe kama chai kisha ipua na uchuje na usubiri ipowe iwe ya uvuguvugu kidogo.
*Sasa changanya pamoja asali nusu lita, juisi au maji maji ya limau nusu lita, maji ya uvuguvugu ya mdalasini lita 2 na nusu ongeza na ya maji ya kawaida lita 1 kupata lita 5, chuja vizuri. Ihifadhi katika friji isiharibike.
Kunywa robo lita (ml 250) kutwa mara 2 kwa siku 10 kwa mtu mzima na glasi ndogo moja kwa siku kwa mtoto wa miaka miwili mpaka kumi.
Unaweza pia kuongeza majani kidogo ya mnanaa (mint) na mbegu za shamari (fennel seeds) ili kuongezea radha na harufu nzuri. Kunywa juisi hii kila unapokuwa umepata chakula cha mchana cha nguvu au cha jioni.
2. MAZIWA YA MTINDI
Mtindi au bidhaa zitokanazo na maziwa ya mtindi, ni tiba ya kuaminika ya fangasi wa ukeni. Unaweza kutumia njia yeyeote kuweka maziwa ya mtindi au yogati kiasi kidogo labda kijiko kidogo cha chai ukeni wakati wa kulala na asubuhi unajisafisha kama kawaida.
Pia inashauriwa kula tu huu mtindi kiasi cha kutosha kila siku.
Uke wenyewe una uwezo wa kuondoa mabaki yote ya mtindi na kubakisha kiwango kikubwa cha bakteria wazuri (lactobacillus) pamoja na hali ya tindikali yenye uwezo wa kuzuia kujitokeza na kukua kwa fangasi. Bakteria hawa wanaopatikana katiaka mtindi hukusanywa viwandani na huuzwa kama bidhaa ijulikanayo kwa kitaalamu kama “Supplements of Acidophiles”.
3. KITUNGUU SWAUMU
Kitunguu swaumu kina sifa na uwezo wa kuua bakteria na hata virusi mwilini.
Chukuwa kitunguu swaumu kimoja
Kigawanyishe katika punje punje
chukua punje 6
Menya punje moja baada ya nyingine
Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo sana na kisu na uache hivyo katika hewa kwa dakika 10
Meza kama unavyomeza dawa na maji nusu lita kila unapoenda kulala. Namna nyingine nzuri zaidi ni kuviweka ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi freshi koroga vizuri na unywe na hii itakusaidia kupunguza harufu mbaya ya kitunguu swaumu huku ukipata faida nyingine mhimu zilizomo kwenye mtindi.
Meza kama unavyomeza dawa na maji vikombe 2 kila unapoenda kulala na asubuhi ukiamka tu.
Fanya hivi kila siku kwa wiki 2 hadi tatu. Mama mjamzito chini ya miezi 4 ni vema asitumie, kwa ujumla tu mjamzito uwe makini utakapotumia kitunguu swaumu kwa namna hii kama wewe ni mjamzito.
4. MAFUTA YA NAZI
Kama fangasi hao wa ukeni wanajitokeza hadi sehemu kidogo ya nje ya uke na unapata muwasho pia, hakikisha unapakaa mafuta ya asili ya nazi yaliyotengenezwa nyumbani. Hii dawa tosha kwa fangasi wowote juu ya ngozi.
MAMBO MHIMU YA KUZINGATIA:
Fangasi hii inaweza ikachelewa kupona au ikawa inajirudia hata baada ya kupona kama hutazingatia yafuatayo:
*Kunywa maji mengi kila siku kuanzia glasi 8 hadi 10
*Punguza vyakula vyenye wanga
*Acha kutumia sukari na badala yake tumia asali
*Acha vinywaji baridi, acha pia chai ya rangi na kahawa
*Acha matumizi ya pafyumu hasa maeneo ya huko
*Acha kutumia vidonge vya uzazi wa mpango, hii ni kwa sababu vidonge hivi vinasemwa huwa vinasababisha kushuka kwa kinga ya mwili na kukufanya mrahisi kupata maambukizi ya fangasi.
*Epuka mapenzi kinyume na maumbile

Wednesday, September 13, 2017

jinsi karoti inavyosaidia afya kwenye mwili wa mwanadamu.


KAROTI
TATUA MATATIZO KWENYE MWILI WAKO KWA KUTUMIA KAROTI,
KAROTI HUTIBU MATATIZO YAFUATAYO,
·         Kulainisha tumbo
·         Inapigana na kutibu upungufu wa damu
·         Uvimbe wa saratani
·         Baridi yabisi
·         Kusafisha damu
·         Vidonda vya tumbo
·         Kutibu chunusi
·         Macho
·         Koo
·         Kibofu

MATAYARISHO
Chukua karoti kilo moja ponda au twanga iwe laini chemsha dakika 15 ndani ya maji lita 1au mbili , chuja kunywa juice yake kwavidonda vya tumbo na saratani ya tumbo au saratani ya kizazi tumia nusu kikombe cha chai miezi 3 mpaka 6.
Kwa ajili ya kurembesha uso, nawia juisi yake kila asubuhi mfululizo kwa siku tano

Monday, September 11, 2017

JINSI YA KUZUIA VIRUSI VYA UKIMWI NDANI YA MASAA 72 BAADA YA KUHISI UMEAMBUKIZWA.

Kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi kumeendelea kuwaweka mahali pagumu sana watumishi wa afya kwani siku za usoni wengi wao wataambukizwa na kufa kwa ukimwi kutokana na kazi yao ya kushika damu mda mwingi  wakati wa kazi.. wengi wao hujikata na nyembe za kufanyia upasuaji, kujichoma sindano na kugusa damu kwenye ngozi wakati wanawahudumia wagonjwa wa aina mbalimbali ambao wanaenda kutibiwa kwenye vituo vya afya, mimi mwenyewe nimeshuhudia madaktari wakijichoma au kujikata na nyembe wakati wakifanya uparesheni kubwa kwa watu ambao inafahamika kabisa wameathirika.

  Miaka ya hivi karibuni kuna tumaini kwa watumishi hawa na watu wengine ambao wako nje ya sekta ya afya kujizuia na virusi vya ukimwi baada ya kugundulika dawa za ARV’s ambazo sio tu zinapunguza makali ya virusi vya ukimwi ila vina uwezo wa kuzuia ukimwi kama ukivitumia masaa 72 au siku tatu baada ya kuhisi kuambukizwa. 

Namaanisha nini naposema kuhisi kuambukizwa?
kujichoma na sindano au wembe wakati unahudumia mgonjwa muathirika.
kubakwa na mtu ambaye afya yake haifahamiki.
kufanya ngono na mtu bila kinga kisha ikathibitishwa kwamba mtu huyo uliye lala naye  ni muathirika.
                                                                                                                 
Nini cha kufanya?
Nenda kituo chochote cha afya au hospital ya serikali na waelezee kilichotokea ndani ya masaa 72 baada ya ajali hiyo, kwanza watakupima kujua afya yako na kama ni muathirika tayari wa siku nyingi hautapewa dawa hiyo ila utaanza ushauri ili uanze matibabu{ kama ukiambukizwa leo vipimo huonyesha baada ya miezi mitatu] na kama bado hujaathirika utapewa dawa hzo uzitumie kwa mwezi mmoja{LAMIVUDINE, ZIDOVUDINE na NIVERAPINE} ambazo zitakukinga kwa asilimia mia moja kwa kuzuia virusi kushindwa kuingia ndani ya seli na kuzaliana. kumbuka masaa 72 yakipita dawa hii haitafanya kazi yeyote.. Baada ya miezi mitatu utenda kupima kuhakikisha afya yako.

Watumishi wa afya pia wanamiongozo yao ya kupata dawa hizo kama wakipata ajali hizo maeneo ya kazi, hawa wote wanafahamu utaratibu sina haja ya kuongelea hapa.

Ukweli ni kwamba dawa za ARV zinaweza kutumika kama kinga kwa  watu ambao hawaja athirika kabisa kama wangekua wanazimeza kila siku, tatizo ni kwamba zina madhara makubwa sana ikiwemo kuharibu figo na maini kabisa.

Faida 11 za Kunywa Maji Yenye Ndimu Kila Asubuhi

Faida #1: Huchochea Mmeng’enyo wa Chakula Tumboni

Maji yenye ndimu husaidia chakula kusagika vizuri na haraka katika mfumo wa chakula. Japo limao lina asidi(acid) lakini likiwa tumboni huwa alkali (alkaline) na kufanya mazingira mazuri kwa usagaji wa chakula.
Pia maji ya uvuguvugu husaidia kusawazisha utumbo uliojikunja na kutoa mawimbi tumboni na kufanya chakula kusukumwa vizuri.

Faida #2: Huboresha Kinga za Mwili

Vitamini C na potasiumu iliyomo kwa wingi katika limao inasaidia katika utengenezaji wa seli za kinga katika mwili.

 Faida #3: Husaidia Unyonywaji wa Madini Mwilini

Vitamini C iliyomo katika limao husaidia kunyonywa kwa madini mwilini hasa madini ya chuma ambayo ni muhimu kwa utengenezaji wa damu. Hata kama maji ya ndimu yakiwa baridi.

Faida #4: Husaidia Kinga Dhidi ya Saratani

Vitamini C ni antioksidant (antioxidant) ambayo inasaidia kuondoa free radicalsmwilini ambazo zimetambulika kusababisha saratani (cancer).

 Faida #5: Husaidia Kupunguza Hatari ya Kiharusi

Kutokana na matokeo ya kitafiti ulaji wa matunda jamii ya limao(citrus fruits) inasaidia kupunguza hatari ya kupatwa na shambulio la kiharusi aina ya ischemic(ischemic stroke) hasa kwa wanawake.

Faida #6: Usafishaji wa Mwili na Damu

Limao husaidia kusafisha damu kwa kuondoa uchafu. Limao pia husafisha figo ,ini na mfumo wa chakula.

 Faida #7: Kurekebisha Sukari katika Mwili

Limao husaidia kuweka kiasi cha sukari tumboni na katika mwili kuwa katika kiasi stahili.
Hii inawasaidia sana wagonjwa wa kisukari katika ulaji wao.

Faida #8: Dawa ya Kikohozi na Mafua

Limao ikitiwa katika maji ya uvuguvugu na asali husaidia sana katika kutibu mafua na kikohozi kwa njia ya asili.

Faida #9: Inasaidia Urekebishaji wa Ngozi na Kupona Makovu

Limao inasaidia kufanya ngozi isizeeke. Kama unataka kubaki kijana basi limao litakusaidia.
Tabia za vitamin C za kusafisha uchafu zinasababisha kufanya ngozi kuwa na afya na kutozeeka haraka.

 Faida #10: Husaidia Kupungua Uzito

Limao hupunguza hamu ya kula. Na inajulikana kuwa sababu kubwa ya watu kuwa na uzito mkubwa ni kula chakula kingi au kula mara kwa mara. Limao litakufanya ujisikie kushiba muda mrefu hivyo kusaidia wale amabao wanataka kupungua uzito.

 Faida #11: Kuondoa Harufu ya Mdomo

Limao husaidia kuua bakteria wabaya mdomoni ambao husababisha harufu mbaya.

 Anza Siku Kwa Kunywa Maji yenye Ndimu Kila Siku

Ni zoezi rahisi na haraka kabisa, weka maji yenye joto kidogo (vuguvugu) katika glasi au kikombe , kata limao au ndimu vipande viwili na kamua kipande kimoja tu ndani ya glasi yenye maji.
Kunywa na uanze siku mpya. Ni vizuri ukafanya hivi dakika 30 kabla ya kula chochote kingine kwa faida zaidi.
Anza leo kwa kunywa maji yenye ndimu kila siku asubuhi na uone mabadiliko ndani ya mwili wako. Mshirikishe mwenzio ili naye afaidike.

Sunday, September 10, 2017

SABABU KUMI ZA KUISHIWA AU KUKAUKIWA MAZIWA KABISA KWA MAMA ANAYENYONYESHA

SABABU KUMI ZA KUISHIWA AU KUKAUKIWA MAZIWA KABISA KWA MAMA ANAYENYONYESHA
zifuatazo ni sababu
matumizi ya dawa za uzazi wa mpango; wanawake wengi hutumia njia hizi baada ya kujifungua bila shida yeyote lakini kuna baadhi yao njia hizi huingilia mfumo wao wa kutoa maziwa hasa zikitumika kabla mtoto hajafikisha miezi sita. hii husababishwa na kuongezeka kwa homoni za uzazi yaani progesterone na oestrogen ambazo hushusha homoni ya kutoa maziwa yaani prolactin hormone.kama umekumbwa na hali hii basi acha mara moja njia hiyo na utumie njia zingine kama kondom,kalenda au njia nyingine isiyotumia dawa.
matatizo ya kimaumbile; baadhi ya wanawake matiti yao hayakukamilika wakati wamakua yaani yanakua na upungufu wa vitu muhimu vinavyohifadhi maziwa kwenye matiti kitaalamu kama grandular tissues hii hufanya maziwa yatoke kwa shida sana.mama anashauriwa akamue maziwa wakati wa kunyonyesha na mara nyingi mtoto wa pili mpaka watatu wakizaliwa matiti haya yanakua yameshazoea hivyo hayasumbui tena kutoa maziwa.
upasuaji wa matiti; kama mama ameshawahi kupasuliwa matiti yake kwa shida yeyote labda majipu, ajari, upasuaji wa kuongeza au kupunguza matiti basi kwa namna moja au nyingine hii inaweza kuharibu mfumo wake wa matiti kupitisha maziwa na kujikuta hatoi maziwa ya kutosha.ukiwa na shida hii utahitaji kutumia maziwa mbadala kwa mtoto.
matumizi ya dawa; wakati wa kunyonyesha mama anaweza kuugua na kutumia dawa fulani fulani ili apone ugonjwa alionao lakini kuna baadhi ya dawa ni hatari kwani hushusha kiwango cha maziwa. mfano dawa za kama bromocriptine,methergine,pseudoephredine.
matatizo ya homoni za uzazi; matatizo ya homoni kua juu sana au kua chini sana yanaweza kusababishwa na magonjwa ya ovari, kisukari na kadhalika. pia magonjwa yeyote ya homoni yanayochelewesha mtu kupata mimba huweza kuzuia maziwa pia. ni vizuri ukaonana na daktari kupima kiwango cha homoni na kupata matibabu.
kutonyonyesha usiku; wakati wa usiku homoni inayohusika na kutengeneza maziwa yaani prolactin hutengenezwa kwa kiwango cha juu sana lakini pia ili mtoto alale usiku mzima bila kusumbua lazima anyonye vizuri usiku.kutonyonyesha usiku hupunguza homoni hii na kumfanya mama atoe maziwa kidogo sana siku inayofuata.
kutonyonyesha vya kutosha; kawaida mama anatakiwa anyonyeshe angalau mara kumi ndani ya masaa 24, sasa mwili hutengeneza maziwa unapohisi matiti hayana kitu na kama mwili ukihisi matiti yana maziwa muda mwingi basi unajua maziwa hayahitajiki sana na kuanza kupunguza kiasi cha kutoa maziwa.
kutokula vizuri;maziwa anayotoa mama yanatengenezwa na chakula anachokula wala sio miujiza fulani hivyo kipindi hiki mama anatakiwa ale mlo kamili yaani matunda, protini ya kutosha, wanga, mboga za majan na maji mengi i na ikiwezekana atumie virutubisho vinavyotengenezwa maalumu kwa ajili ya kuongeza maziwa.
matumizi ya vyakula mbadala; miezi sita baada ya kuzaliwa mtoto anatakiwa anyonye tu bila kupewa kitu chochote, kuna watu hua wanawapa maji wakidai eti watoto walisikia kiu sio kweli.sasa kuanza kumchanganyia maziwa ya ngombe na yale ya dukani kutamfanya anyonye kidogo kwako na mwili utapunguza kiasi cha maziwa yako...hivyo siku ukikosa mbadala utajikuta huna maziwa kabisa.
mtoto kushindwa kunyonya; kama nilivyosema hapo mwanzo kwamba maziwa yakitoka mengi na mwili unatengeneza mengi zaidi na kama mtoto hanyonyi vizuri basi na maziwa hutoka kidogo zaidi.hali hii inaweza kusababishwa na dawa ya usingizi ambayo alipewa mama wakati wa kupasuliwa ambayo huamuathiri mtoto pia, au matatizo ya kuzaliwa nayo kama tongue tie[ulimi kushikwa chini ya mdomo, hii inaweza kurekebishwa na daktari] au mtoto kuugua.

MADHARA YA UPIGAJI PUNYETO, NAMNA YA KUEPUKA, NA TIBA

MADHARA YA UPIGAJI PUNYETO, NAMNA YA KUEPUKA, NA TIBA 
Watu wengi sana wanataka kufahamu jinsi gani wafanye ili kuachana na kitendo cha upigaji punyeto. 
Punyeto ni tendo la mtu la kuamsha hisia za mapenzi au msisimko ambao unampelekea mtu huyu kufikia kilele cha kujimalizia tamaa zake! Bila kufanya tendo halisi, hutumia fikra zake katika picha za zinazoitwa za ngono au picha zozote zinazoweza kulifanikisha tendo hilo, movie n.k. Kilele cha yote anafikia mahali anajimalzia tamaa zake mwenyewe!. Nimekuwa nikiona baadhi ya watu wanaosema wameelimika wakipingana wao kwa wao katika suala zima la kupiga punyeto! Wako wanaotetea kutokana na elimu yao na wanasema kwa ujasiri mkubwa kwamba "kupiga punyeto ni sehemu ya maisha ya mwanadamu" Ina maana katika maisha ya mwanadamu upigaji punyeto inaelezwa ni kama tendo la lazima mpaka inafikia mahali wanasema ni sehemu ya maisha (Maisha) ya mwanadamu. 
Nimekuwa nikipata kesi nyingi sana juu ya madhara yatokanayo na punyeto. Aslimia 60 ya vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 30 wameathirika na tatzo hili (chronic masturbation) na inakuwa ngumu kujinasua kutoka kwenye hili janga, kama wewe ni mmoja wapo na ulkuwa ukitafuta kwa mda mrefu ufanye nini ili uachane na tabia ya kupiga punyeto basi fatilia kwa makini makala hii. 
MADHARA YA UPIGAJI PUNYETO KWA MWANAUME 
Haya ndio baadhi ya madhara ya kimwili ambayo yanaletekezwa na upigaji punyeto 
1. PUNYETO INAUA NGUVU ZA KIUME: 
Upigaji wa punyeto unaweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume, kwani kipindi unapiga punyeto jua ile mishipa inayofanya uume usimame unakuwa unaichua na uume unakuwa umesimama kwa muda mrefu sasa ikitokea ukawa unafanya hivi kila siku ile mishipa inalegea na uume unakuwa unakosa nguvu hata ukisimama haui strong unakuwa kama umelegea. 
2. KUWAHI KUMALIZA MAPEMA KATIKA TENDO: 
Mara nyingi mtu aliezoea kupiga punyeto huwahi kumaliza mapema pindi akiwa anafanya tendo la ndoa na wakati mwingine uume hushindwa kusimama kwa mara ya pili na kujikuta anashindwa kurudia tendo ikiwa mwenzake bado hajaridhika na anahitaji kuendelea kufanya tendo hilo. 
Athari nyingine ni kama zifuatazo 
3.Uchovu wakati wote / Fatigue. Feeling tired all the time. 
4.Maumivu ya nyonga / Lower back pain. 
5.Kusinyaa kwa Nywele / Nywele kunyonyoka / Thinning hair / Hair Loss 
6.Maumivu ya kende
7.Maumivu ya kiuno 
Hayo ni baadhi ya nukuu zangu! 
Kuna faida nyingi sana ambazo utazipata endapo utaachana na tabia ya upigaji punyeto na hiyo napenda iwe sababu ya wewe msomaji kuachana hicho kitendo. 
Kuacha punyeto ama mtindo flani wa maisha inahitaji utambuzi, uamue na pia uweze kjicontrol wewe mwenyewe, inahitaji nguvu ya ndani yako kushinda vishawishi , zifuatazo ni njia ambazo utaanza kutekeleza ukiwa nyumbani kwako bila gharama yoyote na zitaanza kukupa matunda, lazima uwe mwaminifu kufuata kile ninachoelekeza maaana ni njia ambayo imewasaidia vijana wengi. 
1.PATA MDA MWINGI WA KUPUMZIKA 
Baada ya shuguli za kawaida haikisha unapata mda wa kupumzika, lala mapema ili uweze kuipa akili mda wa kuchambua na kutunza taarifa za muhimu na kufuta zile ziszo za muhimu. Hakikisha unalala mapema hapo ndipo utaongeza uwezo wa akili kuweza kupambana na hisia na mawazo mabaya. 
2. MATUMIZI YA MBOGAMBOGA NA MATUNDA KWA WINGI 
Utafiti wa kisayansi unaonesha kwamba matumizi mazuri ya vyakula vya mbogamboga na matunda Husaidia kuongeza uwezo binafsi wa kujisimamia juu ya tamaa na mihemko mbalimbali, matumizi ya vyakula vilivyosindikwa (junk foods) ni chanzo cha kushindwa kujizuia na hapo safari yako ya kuachana na upigaji punyeto itakwama. 
3. FANYA MAZOEZI NA USHUGULISHE MWILI 
Maozezi yanasaidia mwili kutofikiria kufanya mambo machafu sababu mara nyingi unakuwa bize, akili inapokuwa inashugulishwa basi uwezekano wa kuleta fikra mbaya ni mdogo sana 
4. ACHA KUANGALIA PICHA ZA NGONO
Tafiti zinasema kwamba vijana wengi wenye umri kuanzia miaka 15 mpaka 30 ndo kundi kubwa lililoathirika kwa kutazama picha za pono, piacha au video za ngono huleta msukumo kwenye akili ili kuweza kujiridhisha na hivo hupelekea watu kupiga punyeto ili kukata ile kiu ya  tamaa zao za mwili